WATANZANIA TUWACHANGIE WENZETU WA KILOSA

WATANZANIA KWA WATANZANIA PAMOJA TUNAWEZA
HARAMBEE YA WAHANGA WA MAFURIKO
Tunaendesha kampeni ya kusaidia wahanga wa mafuriko yaliyoikumba Tanzania tangu wakati wa Siku Kuu ya Krismasi 2009 ambapo maelefu ya watu (hadi sasa zaidi ya 30,000) wameathirika kwa kukosa makazi, vyakula, na huduma za afya na kupoteza mali nyingi. Hadi sasa idadi ya waliokufa inakadiriwa kufikia 10 huku mlipuko wa magonjwa yatokanayo na maji machafu kama Kipindupindu na Typhoid ukianza kuonekana. Harambee hii inahusu kuwasaidia wananchi wenzetu ambao wako katika hali ngumu kutokana na athari za mvua kubwa na mafuriko.
Mafuriko haya hadi hivi sasa yamegusa mikoa ya Morogoro, Dodoma, Shinyanga, Mwanza, Ruvuma, na kwa vile mvua zinaendelea kunyesha kuna uwezekano wa maeneo mengi zaidi kuathirika.
Kwa kushirikiana na mitandao ya www.JamiiForums.Com, www.Issamichuzi.blogspot.com na taasisi ya Wanataaluma wa Tanzania TPN (www.tpntz.org) , Mtandao wa Habari, Burudani na Harakati za kisiasa wa www.mwanakijiji.com unaratibu harambee ya kuchangia wahanga wa mafuriko haya kwa kukusanya misaada ya vitu mbalimbali kwenda kwenye ofisi za Chama cha Msalaba na Mwezi Mwekundu cha Tanzania kuanzia siku ya Alhamisi Januari 14, 2010 na Ijumaa Januari 15, 2010. Chama cha Msalaba Mwekundu ndio chombo ambacho kiko mstari wa mbele kuongoza juhudi za kusaidia walioathirika ikishirikiana na taasisi mbalimbali binafsi na vyombo vya serikali.
Kutokana na rekodi yao ya kukabiliana na majanga, TRC Society ndiyo chaguo letu la kushiriki katika kufikisha misaada kwa Watanzania wenzetu. Tumehakikishiwa na Katibu Mkuu wa Chama hicho Mstahiki Meya wa Jiji la Dar Alhaji Adam Kimbisa kuwa misaada yote inayofikishwa kwa chama hiki hutumika kwa ajili ya yale yaliyokusudiwa.
MISAADA INAYOHITAJIKA :
Kwa mujibu wa Mkuu wa Kitengo cha Maafa cha Chama cha Msalaba Mwekundu Bw. Joseph Kimaryo ambaye KLHN imefanya naye mahojiano (unaweza kusikiliza HAPA au kusikiliza kupitia http://www.podomatic.com/mwanakijiji ) mahitaji makubwa hivi sasa ni:
Magodoro
Mahema
Vyandarua
Vyakula (visivyoharibika)
Maji safi (masanduku ya chupa za maji)
Madawa ya kuzuia maambukizi (ambayo hayajaharibika au kufunguliwa)
Vifaa kwa ajili ya matumizi ya kina mama na watoto
Makaratasi ya kujipangusia (clean wipes)
Fedha kwa ajili ya kugharimia usafirishaji na ufikishaji misaaa kwa walengwa.
MISAADA YAWEZA KUFIKISHWA KWA NJIA ZIFUATAZO
1. Misaada itakapokelewa katika makao makuu ya Msalaba Mwekundu Jijini Dar-es-Salaam na katika matawi ya Red Cross mikoani pote. Hakuna msaada mdogo au usio na maana na Chama kitapokea misaada ya aina zote. Misaada ya fedha na vitu yaweza kupokelewa kwenye ofisi YOYOTE ya Chama cha Msalaba Mwekundu Tanzania.*
Tanzania Red Cross Society
Mrokao Street/Coral Lane (Karibu na Kora Beach Hotel, barabara ya kwenda Chole) Dar es Salaam Postal Address P.O. Box 1133 Dar es Salaam
Kupata maelezo ya matawi ya Msalaba Mwekundu nchini
Mkuu wa Kitengo cha Maafa : Bw. Joseph Kimaryo 713-325042
Contact Information Tel: (00255) (22) 2150330/2151839/2150843 Fax: (00255) (22)2600156 E-Mail: logistics@raha.com
2. Misaada yaweza kukusanywa kupitia Tanzania Professionals Network (TPN) ambao kwa kupitia wanachama wake wataunganisha misaada yao na kuiwasilisha TRC kuanzia Alhamisi.

Mr. Emmanuel Mmari TPN Finance and Administrative Manager Tanzania Professionals Network TOHS Building - Dar Group
1st Floor Nyerere/Mandela Road P.O. Box 21605 Dar Es Salaam, Tanzania
Fax Line: + 255 - 22 - 2115 571 Mobile: +255-715 740 047 Mobile: + 255-754 833 985 E-Mail: president@tpn.co.tz
MICHANGO YA FEDHA*
3. Michango ya fedha ambacho ni kitu muhimu sana kwenye kupambana na majanga haya tutakusanya kwa kupitia njia mbili. Kwenda moja kwa moja kwa Red Cross na njia ya pili ni kupitia TPN. Wao TPN watatumia zaidi mitandao ya simu katika kuchangisha kwa mtu yeyote anayetaka kuchangia kiasi chochote kuanzia Shilingi 150 kwenda juu. Tunajaribu kuzungumza na mitandao mikubwa ya simu ili kuweza kupunguza au hata kuondoa ada ili kuhakikisha kiasi cha juu zaidi kinakusanywa na "Watanzania kwa Watanzania". Michango hiyo itachangwa kupitia namba maalum ambazo tunatumaini kuwa zitakuwa tayari ikifika Jumatatu.
Kwa kupitia TPN watu wataweza kuchangia fedha kwa njia hizi (taratibu zikikamilika tu)*
1. Bank Transfer au Deposit (USD Accounts CRDB)*
2. Bank Transfer au Deposit (TZS Account CRDB)
3. Western Union (Tutawapa jina kamili la Treasurer wa TPN)
4. Kulipia Ofisi za TPN
5. Z-Pesa
6. M-Pesa
7. Zap ya Zain
4: Kwa kutumia kadi za Kibenki kwa walio USA na sehemu nyingine ambazo kadi hizi hutumika (Visa, MasterCard, Discovery na America Express) kupitia mtandao wa www.mwanakijiji.com , upande wa kulia chini kuna mahali panapicha hiyo ya "donate". Michango yote itakayoingia wiki hii ni kwa ajili ya kusaidia wahanga wa Mafuriko. Fedha yote tutakayokusanya wiki hii (ukiondoa ada za PayPal) kupitia mtandao huu tutatuma kwa Bw. Issa Michuzi ambaye ataiwasilisha kwa niaba yetu huko Red Cross Society. Kiasi chochote kinakaribishwa.
5: Kwa watu ambao wana vitu (ukiondoa pesa) ambavyo wangependa kuvifikisha TPN au Red Cross lakini hawana usafiri au uwezo wa kuvifikisha huko hasa katika Jiji la Dar TPN imejitolea mtu wa kuvifuata vitu hivyo na kama kuna mtu mwingine yoyote ambaye anaweza kujitolea usafiri tafadhali wasiliana na TPN kuona jinsi gani wanaweza kutumia huduma yako .
Kwa wale wenye vitu tafadhali wasiliana na TPN ukielezea mahali ulipo na vitu ulivyonavyo ili mipango ya kuweza kufuatilia ifanyike. Taarifa hizo zifikishwe kwa TPN ifikapo Jumatano tarehe 13 Januari, 2010.
Taarifa za ziada zitapatikana Jumatatu:
Wasialiana nami:
M. M. M. Mwanakijiji
KLHN International
Detroit, Michigan, USA
(248) 556 6748
email: mwanakijiji@mwanakijiji.com
* Taarifa zaidi ya akaunti za Benki za TPN na Chama cha msalaba Mwekundu zitapatikana ifikapo Jumatatu Tarehe 11 Januari, 2010

CHANZO CHA HABARI http://issamichuzi.blogspot.com/









Meshack Maganga 2009
Previous
Next Post »

MAONI ConversionConversion EmoticonEmoticon