Na:
Meshack Maganga-Iringa.
Ndugu zangu,
Jumapili ya juzi, nilisoma makala ya mwandishi maarufu
Freddy Macha kwenye gazeti la Mwananchi Jumapili tarehe 11 yenye kichwa ‘Maisha Bongo,Majuu hali moja’. Kwenye
makala yake Freddy Macha ameeleza waziwazi kwamba wapo baadhi ya vijana wa
kibongo ambao huota kwenda kuishi ‘majuu’ bila kujua kwamba huko maisha ni
magumu kuliko hata bongo,na kwamba, popote pale unapoishi utawakuta watu
wakilalamika na kusema kuwa afadhali kwenda mahali pengine. Kisha akaenda mbali
kwakusema kuwa, ukijua na kutambua la kufanya na namna ya kumudu
maisha,unaendelea na mapambano,kwa sababu kanuni kuu ya uhai ni harakati.
Mtanzania
anaweza kuwa na ndoto ya kwenda huko majuu na kichwani kwake akaamini
kwamba akienda majuu 'atatoka' asipojiamini na kutambua fursa zilizopo
nchini kwake huyo atakuwa anapishana na 'future'.
Nakumbuka nilipokuwa kidato
cha pili miaka michache iliyopita,baba yangu Mzee Maganga,alipata safari ya
kwenda Uholanzi, kabla ya kuondoka aliniuliza ni kitu gani ambacho ningependa
atakaporudi kutoka Uholanzi aniletee kama zawadi,nilimwambia aniletee vitabu
vya kusoma, baadhi ya ndugu zangu walinicheka maana wao waliomba waletewe
nguo.Baba aliporudi aliniletea kitabu maarufu cha Dr. Nomarn Vincent Peale,
kiitwacho ‘THE POWER OF POSTIVE
THINKING’,kiakili nikuwa mdogo ila kimenisaidia sana katika kujenga mtazamo
sahihi wa maisha.
Ndugu zangu, kila siku
binadamu anagundua mambo mapya ambayo yanamsaidia kumudu kupambana na mwendo na
mabadiliko ya kasi katika maisha. Miongoni mwa ugunduzi mwingi wa hivi karibuni
umekuwa ukihusu mawazo ya binadamu. Ugunduzi huu umesaidia kubadili mitazamo ya
wanasayansi wengi, wakiwemo wale wa fizikia ambao kea muda mrefu wameonekana
kukataa sana maelezo kwamba mawazo yana nguvu kuliko miili yatu.
Kila mmoja wetu ana namna
yake ya kufikiri na hizi namna tofauti za kufikiri ndizo ambazo
zinatutofautisha binadamu. Ni tofauti hizi pia ambazo zinatufanya tuwe na
tofauti katika mafanikio maishani mwetu. Wale ambao wanafikiri vizuri na
kuamini katika kumudu, huwa wanafanikiwa. Wale ambao wanafikiri vibaya na
kiamini katika kushindwa, siku zote huwa wanaanguka.
Huenda ni vigumu kwa mtu
kujua, huku kufikiri vizuri na kuamini katika kumudu ni kupi na pia huku
kufikiri vibaya na kuamini katika kushindwa ni
kupi. Kwa bahati nzuri hayo yote yameelezwa kwenye mada nyingine
zinazohusu kufikiri kitabuni humu. Kwa bahati nzuri zaidi, wataalamu wa masuala
ya mawazo na mafanikio kama John Gray, Vincent Peale, Anthony Robbinins na
wengine, wanabainisha vigezo ambavyo vinaweza kumfanya mtu kutabiri kama maisha
yake yatakuwa ni ya kushindwa hadi mwisho au yatakuwa ni ya mafanikio.
Inailezwa kwamba, kama mtu
akiwa anaamini kwamba kuna watu wengine wa aina Fulani mahali Fulani, ambao
ndio peke yao wanaoweza kufanikiwa na kufika juu kwenye ngazi ya kimapato, mtu
kama huyo hawezi kamwe maishani mwake kuja kutoka kwenye lindi la umaskini.
Hawezi kutoka kwenye lindi
hilo kwa sababu juhudi zake ambazo zingemfikisha mbali zinakuwa tayari
zimewekewa ipaka na imani hiyo, kwamba yeye hahusiki katika kufanikiwa, bali kuna wengine ambao ni
Mungu mwenyewe anayewajua na
aliyewateua. Kwa kufikiri hivo, juhudi yake kubwa katika kutafuta itakuwa ni ile ya kumfanya
asife tu kwa njaa na siyo kuvuka hapo. Kama ujuavyo, tunapoamini kuhusu jambo
Fulani, mawazo yetu hutusaidia kulifikia jambo hilo.
Kwa kuamini hivyo, mazingira
tunayojenga ni yale ya kutusaidia kuishi kwa kupata riziki tu. Hata kama “fuko
la fedha” litadondoshwa miguu mwetu tutalipiga teke na kuliambia “mimi
sikuandikiwa kupata bwana, kuna wenyewe, hali kama hii hujitokeza mara nyingi
sana maishani mwetu. Tunakabidhiwa dhamana kubwa ambayo ingetusaidia sana maishani
mwetu, lakini tunacheza nayo hadi inapotea kwa sababu tu hatuamini kwamba utunastahili
kuitumia kufika juu. Tunaziona nafasi za kusonga mbele, lakini tunaamini
kwamba, hatustahili kuzitumia.
Fursa zikija waziwazi kabia,
tunajifanya hatuzioni kwa kutafuta visingizio mbalimbali ili tusizitumie, kwa
sababu tu, tumeamini kwenye mawazo yetu kwamba, sisi hatustahili. Ni vigumu
kugundua kwamba nafasi au fursa hizo zimekuja kwa sababu tayari tumejifungia
njia kuelekea mafanikio. Wengine kwa bahati baya wanaweza kuona na kubaki
wameshangaa ni kwa nini tushindwa kuinuka katika mazingira tuliyomo.
Mtu ambaye anaamini kwamba
hawezi, yaani ameshashindwa kutokana na sababu mbalimbali, anaelezwa na
wataalamu wa elimu ya mafanikio kwamba, kamwe mtu huyu hawezi kuja kuvuka
kizingiti cha umaskini. Kuna watu ambao kutokana na sababu mbalimbali
walifanywa kuamini kwamba hakun wanchoweza. Wengine kutokanana malezi,
mazingira au uzoefu mbalimbali wa kimaisha.
Mtu anapoamini kwama hawezi,
anayaambia mawazo yake ya kina yamsaidie kumfanya ashindwe zaidi kwenye kila
jaribio analofanya. Badala ya kufanya juhudi kujisaidia ili amudu, hujipweteka
kwa kuamini kwake kwamba hata kama atafanya kitu gani, kamwe hatamudu. Siyo
rahisi kwa mtu mwenye mawazo ya aina hii kuweza kufanikiwa maishani.
Kuna watu ambao kwa sababu
ya kukosa kile ambacho jamii inakiona kuwa ndiyo ufunguo wa mafanikio, huwa
wanaamini kwamba hawawezi kufanikiwa au kufanya vizuri maishani kama hao ambao
wanacho. Kwa mfano, kwa kukosa elimu, ujuzi au utaalamu fulani, watu wengine
hujihesabu kama wanyonge. Huchukulia kwamba ni wale tu wenye elimu, ujuzi na
utaalamu fulani ndiyo wanaoweza au wanaotakiwa kufanikiwa.
Bila shaka umeshawahi
kusikia au hata wewe mwenyewe kusema, “Si wamesoma bwana’ ndiyo wanaojaliwa,
sisi ambao hatuna elimu kazi yetu itakuwa ni kuwatumikia. Kauli kama hizi zina
chimbuko lake mbali sana, pengine katika malezi yetu. Wazazi kwalizoea au
wamezoea kuwaambia watoto wao, “Usiposoma kazi yako itakuwa ni kuwabebea
wenzako mizigo, unafikiri pesa inaokotwa, nk. Kwa bahati mbaya mtoto aliyelishwa “sumu” (‘EARLY CHILD PROGRAMMING’) hii
anaposhindwa shule, huamini kwamba yeye atabaki kuwatumikia wengine tu.
Tunapoamini kwamba kwa sababu
hatuna elimu ya kutosha napengine ujuzi au utaalamu Fulani, hatuwezi kufika juu
kwenye mafanikio, ni wazi hatutafika. Moja ya vigezo muhumu vinavyoweza kutufikisha kwenye mafanikio ni kuamini kwetu
kwamba tunaweza kufika huko. Tunapokuwa hatuna imani kwamba tunaweza kufika
huko hujifungia njia wenyewe.
Baadhi yetu kuwa tunaamini
kwamba tuna mikosi, balaa au nuksi napengine laana ambazo zinatuzuia katika
kufikia malengo yetu. Tunaamini hivyo kiasi kwamba hata tukifikia karibu kabisa
na mafanikio huwa tunajiambia ni kazi bure, tutaporomoka tu. Na kweli kwa
kuamini hivyo hujikuta tukiporomoka kila tukifika karibu na kufanikwa au kufikia
malengo.
Kinachotokea ni kwamba, kwa
kuamini kwetu kuwa tunamkosi, balaa, laana au nuksi, huwa tunatenda kwa mkabala
huo wa kinuksi au kibalaa na kimkosi, ambapo matokeo yake ni kujikwamisha.
Watalaamu wa elimu ya mafanikio wanaeleza kwamba tunapoamini kuwa tuna mkosi au
nuksi huwa tunayashauri mawazo yetu ya kina kutusaidia kuendelea kuwa katika
hali hizo (Niliwahi kufafanua zana hii nilipoandika makala ya BINADAMU NI ZAIDI YA
MWILI WAKE). Ndiyo maana siyo rahisi
kukuta mtu anayeamini katika nuksi akiondoka katika hali hiyo.
Tufanyeje basi, kama ni
kweli kimapato tuko hoi napengine tunachoweza ni kupata riziki yetu ya kila
siku tu? Pamoja na kwamba mengi yameelezwa
tayari kwenye mada nyingine, bado tunaweza kukuambia, tunachotakiwa
kufanya ni kujenga imani ya kumudu. Kamwe hatutakiwi kabisa kujiambia
tulipofikia ndipo basi, hatuwezi kupanda zaidi.
Mwaka 1997, Pablo alikuwa ni mtu wa
kuishi kwa kubahatisha. Alikuwa akifanya vibarua hapa na pale na maisha
yalikuwa magumu sana kwa upande wake. Hakuwa na matumaini kabisa kwamba
ingetokea siku akasimama. Siku moja akiwa kwenye kibarua chake, alimsikia mtoto
wa tajiri yake akisema, “Baba
haiwezekani, tusikate tamaa ni Lazima tutaweza, kwani wanaoweza wana mkataba
gani na Mungu?, ni lini waliongea na Mungu na kuhakikishiwa kwamba wangekuja
kupata?. Tujipe moyo wa kuweza halafu tufanye…” ITAENDELEA.
meshackmaganga@gmail.com
Sign up here with your email
1 comments:
Write commentsUkweli ulio uchi
ReplyMAONI ConversionConversion EmoticonEmoticon